Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 23, 2018 itatoa uamuzi kama Wema Sepetu
na wenzake wawili kama wana kesi ya kijibu au la.
Uamuzi
huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya
kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka na
kuufunga ushahidi wao.
Machi 23, 2018 upande wa utetezi uliwasilisha hoja katika Mahakama hiyo ili waone washtakiwa hao hawana kesi ya kujibu.
Mbali na Wema, wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abbas.
Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.
Inadaiwa
kuwa Februari 4, 2017 katika makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio
washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye
uzito wa gramu 1.08.
Wema
anadaiwa kuwa Februani Mosi, 2017 katika eneo lisilojulikana jijini
Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.
0 comments:
Chapisha Maoni