Mbunge
wa Kojani, Hamad Salim Maalim (CUF) amehoji ni lini Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania itaruhusu Zanzibar kuwa na uwakilishi rasmi
katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akiuliza
swali leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu, mbunge huyo
amedai hatua hiyo ni kwa kuwa mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar
yanaitambua Zanzibar kuwa ni nchi.
Akijibu
swali hilo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dk. Augustino Mahiga amesema Ibara ya pili (1) ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na mabadiliko yake imebainisha
eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote
la Tanzania Zanzibar. Pia ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo
Tanzania inapakana nayo.
“Naomba
kulihakikishia bunge kuwa maslahi yote ya Zanzibar katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki yanazingatiwa ipasavyo,” amesema Mahiga
0 comments:
Chapisha Maoni