Rais
wa Marekani Donald Trump amesema kuwa iwapo mazungumzo yake na kiongozi
wa Korea Kaskazini, Kim Jong un hayatazaa matunda basi ataachana na
mazungumzo hayo.
Katika
mkutano wa pamoja na vyombo vya habari, Trump na waziri mkuu wa Japan
Shinzo Abe wamesema kuwa shinikizo dhidi ya Korea Kaskazini ni sharti
liendelee kwa kukataa kusitisha utengenezaji wa silaha za nyuklia.
Vile
vile, Trump amethibitisha kwamba mkurugenzi wa CIA, Mike Pompeo
alifanya ziara ya kisiri hadi Korea Kaskazini ili kukutana na Kim Jong
Un.
Hata
hivyo, kwa upande wake waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe amemtaka rais
Trump kusaidia kuachiwa huru kwa raia wa Japan waliotekwa nyara na Korea
Kaskazini miaka ya 1970 na 1980.
0 comments:
Chapisha Maoni