Wasanii
wa Bongo Movie wakiongozwa na Steve Nyerere kwa Pamoja wamekwenda
hospitali aliyolazwa muigizaji mkongwe mzee Majuto kwa lengo la kumuona
na kumpa faraja katika kipindi hiki ambapo amelazwa katika hospitali
hiyo.
Pamoja
na kwenda hapo wamemkuta Mzee Majuto yupo kwenye hali nzuri huku
akijitokeza mdau ambaye ni Kampuni ya ASAS aliyejitolea Ticket mbili
kwaajili ya Mzee Majuto kwenda kutibiwa India.
Baada
ya hapo Msanii Steve Nyerere alizungumza na waandishi wa habari na
kusema kuwa'" Ni kweli tumepata ticket mbili za Mzee wetu kwenda
kutibiwa India na siku ya kesho tutakamilisha huo utaratibu wote na sisi
tunajaliana kwenye shida tuache haya makundi ya ajabu ajabu kama
tunataka kutengeneza Industry lazima tukubaliane, wote tuache porojo
hazijengi Industry ila zinakandamiza”
0 comments:
Chapisha Maoni