Goli la Simba lililofungwa na Erasto Nyoni kwenye mchezo wa watani wa jadi lina siri kubwa kama ulikuwa hujui.
Nyoni alitabiriwa na mkewake kuwa atafunga goli dhidi ya Yanga jambo
ambalo limetimia, dakika ya 38 kipindi cha kwanza ambapo aliunganisha
kwa kichwa mpira uliopigwa na Shiza Kichuya.
Nyoni amemshukuru mkewe na familia yake kwa ujumla baada ya kufunga
goli hilo na kuwaomba mashabiki wa Simba waendelee kuisapoti timu hadi
ichukue ubingwa.
“Kabla ya mchezo wa leo (dhidi ya Yanga) mkewangu aliniambia
nitafunga goli kitu ambacho kweli kimetokea nimefanikiwa kufunga”-Erasto
Nyoni.
“Namshukuru mkewangu na familia yangu kwa ujumla kwa kuniombea,
nimefurahi timu imeshinda na kupata pointi tatu. Nawaomba mashabiki
waendeleea kuisapoti timu hadi tuchukue ubingwa.”
Simba imefikisha pointi 62 baada ya kucheza mechi 26 ikiendelea
kuongoza ligi, Yanga inashuka hadi nafasi ya tatu wakiwa na pointi 48
lakini wana mechi mbili mkononi (viporo) nafasi yapili ipo Azam ikiwa na
pointi 49 baada ya kucheza mechi 26.
0 comments:
Chapisha Maoni