Na Mwandishi Wetu – Mwanza
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Idara ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) imesema haitasita
kulifutia usajali Shirika lolote lisilo la Kiserikali litakaloenda
kinyume na Sheria na Taratibu za nchi.
Hayo
yamesemwa jana Jijini Mwanza na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali Bw. Marcel Katemba alipokuwa akifungua kikao kati yake na
Wasajili Wasaidizi wa Mashirka Yasiyo ya Kiserikali na Wadau wa
mashirika hayo kwa Mkoa wa Mwanza.
Bw.
Katemba amesisitiza kuwa kwa mujibu wa Sheria namba 4 ya Mwaka 2002 ya
Mashirika Yasito ya Kiserikali inayataka Mashirika hayo kuzingatia
Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Nchi katika utendaji wa kazi zao
kwa mujibu wa Katiba na majukumu yao kiusajili.
Ameongeza
kuwa kikao hicho kimefanyika ili kuwakumbusha wadau wa NGOs kufanyakazi
kwa kuzingatia Sheria za nchi zilizopo kwani baadhi ya mashirika hayo
yamekuwa yakitumika kufanya mambo ambayo yapo kinyume na Sheria.
“Nawataka
wamiliki wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuzingatia matakwa ya
usajili wao katika kutekeleza majukumu katika Mashirika yao” alisema
Bw.Katemba
Bw.Katemba
amesema kuwa mpaka sasa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 4,868 ndio
yamehakikiwa na kuyataka Mashirika ambayo hayajahakikiwa yafanye
utaratibu wa kuhakiki kwani mara baada ya kuzinduliwa kwa Tovuti mpya ya
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini Mashirika ambayo hayatakuwa
yamehakikiwa hayataruhusiwa kufanya kazi nchini.
Naye
mdau kutoka Shirika la Baraka Orphanage Bi. Patricia Kamugisha asema
kuwa kikao hicho imewasaidia kujifunza mambo mengi ambayo walikuwa
hawajafahamu na kuendelea kupata uzoefu utakaowasaidiza kuimarisha
utendaji wa shughuli katika mashirika yao.
“Sisi
kama wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali tunatakiwa kuzingatia
Sheria na Taratibu zilizopo ili tuweze kufanya kazi bila kukinzana na
Sheria” alisisitiza Bi. Patricia.


0 comments:
Chapisha Maoni