Wanafunzi
wawili wakazi wa Olkeryan jijini Arusha wamefariki dunia baada ya
kutumbukia kwenye shimo lililokuwa likitumika kwa ajili ya ujenzi wa
barabara ya mchepuko inayotoka Ngaramtoni kuelekea Moshono.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo jana Jumatano Aprili 11, 2018
aliwataja wanafunzi hao kuwa ni Hadija Hans aliyekuwa mwanafunzi wa
darasa la pili Shule ya Msingi Olkeryan na Christina Kivuyo mwanafunzi
wa darasa la tano Shule ya Msingi Mt Meru.
Mkumbo
alisema Hadija alikuwa akipita karibu na shimo hilo hilo Jumanne saa
11;30 jioni na kutumbukia na kwamba Kivuyo alipokwenda kwa nia ya
kumsaidia naye alitumbukia katika shimo hilo na wote kufariki dunia.
Amesema
baada ya tukio hilo wafanyakazi wanaojenga barabara hiyo kwa
kushirikiana na wananchi na polisi walienda eneo la tukio na kukuta
miili ya wanafunzi hao, ambayo waliipeleka Hospitali ya Mt Meru.


0 comments:
Chapisha Maoni