Kauli
hiyo imetolewa leo Jumatatu, Aprili 23 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati akitoa ufafanuzi wa hoja za
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kwa
muda sasa kumekuwapo na kelele nyingi kutoka katika maeneo mbalimbali
ikiwemo wadau na wasomi kuwa Jiji la Dar es Salaam ramani yake haifuatwi
na ndiyo sababu kumekuwa na mafuriko ya mara kwa mara.
Hivi
karibuni aliyekuwa waziri katika wizara hiyo, Profesa Anna Tibaijuka
alisema ramani hiyo iliachwa na watu kuanza kujenga kiholela na hivyo
kusababisha mpangilio mbovu wa kuzuia njia za maji na kusababisha
mafuriko mara kwa mara.
“Ni
kweli, master plan ya Jiji la Dar es Salaam hatujaipitia kwa muda
mrefu, ni kama iliachwa, lakini tumeamua kuachana nayo na kutengeneza
master plan mpya na imeshachorwa, lakini kwa sasa inafanyiwa mapitio
pale wizarani kwangu,” amesema Lukuvi.
Waziri
huyo amesema katika utaratibu wa kawaida, ramani za mipango miji
hupitiwa kila baada ya miaka sita, lakini ramani ya Jiji la Dar es
Salaam haijapitiwa tangu wakati huo na hivyo Serikali imeachana nayo na
kuamua kuanza mpango upya.
Akizungumzia
hoja za CAG, Lukuvi alikiri kuwa suala la upimaji na ugawaji wa viwanja
haliendi vizuri kama alivyoeleza katika taarifa yake akitaja sababu za
ukosefu wa watalamu uliokuwepo.
0 comments:
Chapisha Maoni