Wizara ya Afya imesema duniani kote hakuna dawa iliyogundulika kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa kisukari na kupona.
Naibu
Waziri wa Afya, Dk Faustin Ndugulile amesema matibabu yanayotolewa kwa
sasa ni kumpatia mgonjwa kiwango bora cha kuishi na kuhakikisha kiwango
chake cha sukari mwilini kinakuwa ndani ya kiwango kinachotakiwa.
Dk
Ndugulile ametaja dawa hizo ni sindano za insulin ambayo mgonjwa
hulazimika kuchomwa kila siku kwa maisha yake yote pamoja na vidonge
ambavyo humeza kila siku.
Katika
swali la msingi Mbunge wa Viti Maalumu(CCM), Christina Ishengoma
amehoji Serikali ina mpango gani wa kufanya tafiti kuhusu dawa za
kisukari.
Waziri
amesema ugonjwa huo huwapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 35 na
kuendelea ingawa watoto na vijana wanaweza kupata ugonjwa huo kwa
kutozingatia misingi ya lishe.
Amesema
kuna tafiti zinazofanywa duniani kote ili kutafuta dawa itakayoweza
kutibu kabisa ugonjwa huu ingawa tafiti hizo hazijazaa matunda.
0 comments:
Chapisha Maoni