Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amegharamia gharama mbalimbali
katika msiba wa Agnes Gerald alimaarufu kama Masogange ambaye amefariki
April 20, 2018 na kuzikwa leo April 23, 2018 jijini Mbeya.
Akiongea
mbele ya waombolezaji na Mkuu wa mkoa wa Mbeya mchekeshaji maarufu
nchini, Emmanuel Matebe Mathias 'MC Pilipili' ambaye ndiye 'MC' wa
shughuli za mazishi ya Agnes Masogange amesema kuwa wameona mkono wa
serikali katika hilo na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ndiye
aliyefanikisha na kulipia magari ambayo yamewapeleka wasanii mbalimbali
Mbeya.
"Mkuu
wa mkoa wa Mbeya kuna upendo mkubwa ambao tumeuona kutoka kwenu kwani
ulikuwa karibu na sisi muda mwingi, ulikuwa ukitupigia simu kujua tupo
wapi hivyo naamini usiku wa leo hujalala kabisaa.
"Pia
tunamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwani yeye ndiye aliyelipia
magari mawili, matatu ambayo yametuleta hapa Mbeya leo kutokea Dar es
Salaam, hata kamati ambayo ilikuwa imeandaa kuanzia kutoa heshima ya
mwisho pale Leaders Club ambayo ilikuwa chini ya Steve Nyerere ilipewa
nguvu na watu wa serikali tumeona serikali mmetupa support vizuri"
alisema MC Pilipili
Mbali
na hilo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla aliweza kuwapokea na kutoa
neno la shukrani kwa wasanii na watu mbalimbali ambao wameweka tofauti
zao pembeni na kuungana kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha
wanampumzisha salama mwenzao katika nyumba ya milele.
"Mueendelee
kuwa pamoja hivi hivi bila kujali tofauti zenu, mabifu yenu mzidi kuwa
wamoja kwani hili jambo mmejenga heshima kubwa sana, naomba nitoe pole
sana kwa familia kwa msiba huu" alisema Makalla
0 comments:
Chapisha Maoni