Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema
kuwa mtu yeyote ataye jaribu kuuchezea muungano atashughulikiwa vikali
hata kama atakuwa nje ya nchi.
Ameyasema
hayo wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar, ambapo amesema kuwa kuna watu ambao hawapendi
muungano uwepo lakini watu hao ni wa kupuuzwa.
Amesema
kuwa muungano ni kitu kikubwa cha kujivunia hivyo Watanzania wanapaswa
kuunga mkono juhudi zote zinazofanywa na Serikali.
“Muungano
wetu ni mfano wa kuigwa duniani, kwasababu ni muungano wa kihistoria
ambao ndio muungano ambao ni mfano katika mataifa mengine, lakini kuna
watu ambao hata kama mkifanya vitu vizuri wenywe kazi yao ni kubeza tu,
sasa nasema kwa yeyote atayejaribu kuuchezea muungano huu atachuliwa
hatua kali haijarishi yuko ndani ya nchi ama nje ya nchi,”amesema Rais
Dkt. Magufuli
0 comments:
Chapisha Maoni