Rais
wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
amewapa ujumbe mzito watanzania kupitia wakazi wa kondoa mkoani Dodoma
akiwataka wazitumie vizuri mvua zinazonyesha na kuhakikisha
wanajihusisha na kilimo kisawa sawa ili kuepukana na njaa.
Magufuli
aliwataka wananchi kuzitumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha badala
ya kuziona kero kwao huku akisema,hakuna mtu yeyote atakayepewa msaada
wa chakula msimu huu.
Alisema yapo baadhi ya maeneo wananchi hawalimi lakini baadaye wataanza kulia njaa na kuomba chakula.
“Hivi
mvua inanyesha namna hii baadaye uje useme una njaa ,na hii
nawaeleza watanzania wote kuanzia Kongwa mpaka Chato,hakuna atakayepewa
msaada wa chakula.”alisema Magufuli.
Akieleza
zaidi alisema,wananchi wanaoishi kando kando mwa barabara wanapaswa
kuitumiwa katika kukuza Uchumi ili wanufaike na kuwataka wananchi kulima
kwa bidii huku akisema,bila kufanya hivyo barabara hiyo haitawasaidia
Amewasifia
wanawake wanaoishi kandokando mwa barabara katika mikoa ambayo tayari
wanaitumia nafasi hiyo kama fursa na kuwataka wote wanaojidekeza
kusubiri serikali kuwahudumia hasa vipindi vya njaa kwamba
hawatafanikiwa.
0 comments:
Chapisha Maoni