JUMLA
ya akinamama 20,815 waliofanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa
shingo ya kizazi mkoani Pwani katika kipindi cha miaka mitatu kati yao
530 walikutwa na dalili za awali za saratani hiyo,ambapo watatu
walifariki.
Aidha
kati ya akinamama hao waliofanyiwa uchunguzi akinamama 412 walitibiwa
matibabu na 115 walipata rufaa ya kwenda Oceanroad na hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Akitoa
takwimu hizo ,wakati wa uzinduzi wa zoezi la chanjo ya kuzuia saratani
ya mlango wa shingo ya kizazi kwa watoto wenye umri wa miaka 14 ,kimkoa
yaliyofanyika kituo cha afya mkoani,Kibaha,mganga mkuu wa Mkoa wa Pwani
,Yudas Ndungile alisema , ipo changamoto ya kutojua idadi ya vifo kamili
kwa kuwa wengi hupata rufaa.
Pamoja na hayo ,alisema ipo haja ya kuona ukubwa wa tatizo hilo kwa kuangalia afya mapema na watoto wa mashuleni kupata chanjo.
Ndungile
alisema jumla ya watoto wa kike 18,823 waliopo shule na nje ya shule
mkoani hapo watapatiwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
mwaka huu.
Alielezea, tayari wameshapokea chanjo na wataanza kuzitoa katika vituo mbalimbali vya huduma.
Ndungile
aliitoa shaka jamii kuwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
ni salama ,haina madhara na haiathiri uwezo wa binti kupata watoto hapo
baadae
”
Serikali imethibitisha usalama wa umadhubuti wa chanjo ya kukinga
saratani ya mlango wa kizazi ndiyo maana imeiongeza kwenye mpango wa
Taifa wa chanjo ili iweze kusaidia kudhibiti tatizo hilo kwa akinamama”:
Ndungile
alieleza mwaka 2018 chanjo itatolewa kwa wasichana waliofikisha umri wa
miaka 14 na ili kupata kinga kamili walengwa watahitaji kupatiwa dozi
mbili.
Alisisitiza
chanjo hiyo huwakinga wasichana wasipate saratani ya mlango wa kizazi
pindi wawapo watu wazima wakiwa na familia zao.
“Nchini
Tanzania saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza kwa vifo ikifuatiwa
na saratani ya matiti ” Saratani hizi mbili kwa pamoja husababisha zaidi
ya asilimia 50 ya vifo vyote vya wakinamama vitokanavyo na
saratani”alibainisha Ndungile.
Kwa
upande wake ,Mganga mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Dkt.Tulitweni
Mwinuka alisema ,wamezindua chanjo hiyo kwa wasichana wenye umri wa
miaka 14.
Alielezea
,kiwilaya wamezindua chanjo hiyo kwa wasichana 100 kituoni hapo na
wanatarajia kufanikisha na kuleta matokeo kutokana na chanjo hiyo .
Akizindua
zoezi hilo ,kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Pwani,mkuu wa wilaya ya Kibaha
Assumpter Mshama aliwataka wanafunzi wa kike kuacha kujiiingiza kwenye
vitendo vya ngono mapema ili kujiepusha kuingia kwenye hatari ya kupata
magonjwa ya zinaa,ukimwi na hata saratani ya mlango wa kizazi.
Alisema
moja ya sababu zinazosababisha saratani hiyo ni kuwa na wanaume wengi
,kuvuta sigara ,wenye mitala, na kuanza mapema kufanya ngono.
“Acheni
kujiingiza kwenye mapenzi mapema ni hatari katika maisha yenu, ukivua
sketi ,na mwanaume akavua suruali jua kuna hatari ya kuhatarisha maisha
yako kwa magonjwa yanayosababishwa kutokana na ngono”
“Jizuieni hadi hapo mtakapoolewa ,msikimbilie ngono za haraka,mtapata saratani”: alisisitiza Mshama.
Mshama aliwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao wa kike wenye umri wa miaka 14 kupata chanjo hiyo kwani haina madhara.
0 comments:
Chapisha Maoni