Jeshi
la Polisi nchini limesema operesheni zake za kila siku haziwalengi
wafuasi wa chama fulani, bali linakabiliana na wananchi wenye fujo.
Lakini limesema, wakati mwingine mazingira yanapokuwa magumu ni bora jeshi hilo lipate lawama kuliko fedheha.
Akizungumza
leo Aprili 4 katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na televisheni
ya Clouds, Msemaji wa jeshi hilo, ACP Barnabas Mwakalukwa amesema;
“Bora
kupata lawama kuliko fedheha.... maana wakati mwingine mambo
yakiharibika nyie wanahabari ndiyo mnakuwa wa kwanza kuandika vichwa
vikubwa vya habari ‘watu sabini wafa mbele ya askari.”
Mwakalukwa
alikuwa katika kipindi hicho akifafanua kuhusu uzinduzi wa nyumba mpya
za askari utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii mjini Arusha.
Amesema
kuna wakati jeshi hilo linajikuta halina namna zaidi ya kutumia nguvu
kubwa kukabiliana na uharibifu kuliko kuamua kutumia nguvu ya wastani na
baadaye madhara yake yanakuja kuwa makubwa.
Akijibu
swali la mwananchi mmoja aliyetuma ujumbe kwenye kituo hicho na kuhoji;
“ kwa nini jeshi hilo limekuwa likitumia nguvu kubwa kwa wafuasi wa
vyama na hata wakati mwingine kuwasukuma bila sababu”, ACP Mwakalukwa
amesema:
“
Kwanza sisi hatujui kama kuna wafuasi, tunatambua wananchi. Kama wapo
hao wafuasi wanamfuata bosi wao na kumshangilia sisi tunachofanya ni
kuwatawanya wananchi ili wasilete bughudha kwa wengine. Tunachofanya ni
kutumia nguvu za wastani tu kulingana na nguvu tunayokabiliana nayo,”
alisema.
Kumekuwa
na malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa vyama vya siasa
vinavyolishutumu jeshi hilo kutumia nguvu kubwa wakati vyama hivyo
vikiwa katika majukumu ya kisiasa.
0 comments:
Chapisha Maoni