Hotuba
ya Kambi ya upinzani kuhusu bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu, haitasomwa
bungeni baada ya kambi hiyo kuchelewa kuiwasilisha.
Hayo
yameelezwa leo, Aprili 4 na Naibu Spika Dk Tulia Ackson dakika chache
kabla ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kusoma bajeti yake.
“Kwa
maelekezo yaliyotolewa na Spika Ndugai, kwa kambi ya upinzani ni kuwa
upinzani wanatakiwa kuwasilisha hotuba yao siku moja kabla ya bajeti
kusomwa bungeni ili kuondokana na matatizo ya kuchelewa kuzipata hotuba
hizo,” amesema Dk Ackson
Waziri
Majaliwa leo anawasilisha bungeni mapitio na mwelekeo wa kazi za
Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri
Mkuu na Ofisi ya Bunge, kwa mwaka wa fedha 2018/2019 mjini Dodoma.
0 comments:
Chapisha Maoni