Nyumba
12 zilizopo kando ya Mto Msimbazi,Mtaa Majengo Eneo la Vingunguti
jijini Dsm zimesombwa na Maji na huku nyingine zaidi ya 100 ziko
hatarini kuanguka kutokana na Mmomonyoko wa Udongo unatokana na kupanuka
kwa Mto Msimbazi na kuingia katika makazi ya watu.
Baadhi
ya wananchi wanaoishi katika mtaa huo wamesema hali ni mbaya katika
eneo hilo, kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha huku mto huo
ukiendelea kutanuka baada ya kuacha njia yake ya asili na kuingia katika
makazi yao.
Diwani
wa Eneo hilo Omar Kumbilamoto amesema walifanya juhudi za kupambana na
mto huo kwa kuwashirikisha wananchi ambao kiasi cha Million 2
zilichangwa, lakini alidai baadhi ya watumishi katika manispaa
hawakuonyesha ushirikiano na kuomba wizara ya mazingira chini ya ofisi
ya makamu wa rais kuingilia kati.
0 comments:
Chapisha Maoni