Mwanadada
Monalisa ambae ni msanii mkongwe sana katika tasnia ya filamu
amekabidhiwa bendera ya taifa pamoja na ticket ya ndege na Mh waziri wa
michezo Harrison Mwakyembe kwa ajili ya safari yake ya kwenda Ghana
ambapo ataenda kuepeperusha bendera ya Taifa katika maswala ya tasnia ya
filamu kutokana na kuchaguliwa kwake katika kuwania tuzo za African
Prestigious Award nchini humo zitakazofanyika April 14,2018 .
Monalisa
ambae alisindikizwa na mama yake katika makabidhiano hayo katika ofisi
za Baraza walihudhuria pia watu mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa
Habari sanaa na Michezo Mh .Juliana Shonza pamoja na katibu mtendaji wa
baraza la sanaa tanzania.
Monalisa
anakwenda kuiwakilisha Tanzania baada ya kuchaguliwa katika kategoria
hiyo na kuomba watanzania na afrika kwa ujumla kumpiagia kura kwa
kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja sasa.Kila la kheri kwake.
0 comments:
Chapisha Maoni