Rais
wa Marekani Donald Trump amesema kuwa nchi yake imejipanga na iko
tayari kuishambulia tena Syria kama itarudia kufanya mashambulizi ya
silaha za kemikali.
Onyo
hilo la Trump limekuja baada ya Marekani, Ufaransa na Uingereza kufanya
mashambulizi katika maeneo matatu ya Syria ndani ya saa 12, kwa
kufyatua makombora 100.
Marekani
na washirika wake hao wanadai kuwa Syria ilifanya mashambulizi ya
silaha za kemikali wiki iliyopita katika eneo la Douma na kusababisha
vifo vya watu wasio na hatia, kinyume cha sheria za kimataifa.
Urusi
ambao ni washirika wa Syria waliwasilisha hoja katika Baraza Kuu la
Usalama la Umoja wa Mataifa ikitaka kitendo kilichofanywa na Marekani
kulaaniwa vikali na umoja huo, ombi ambalo lilipingwa baada ya mjadala
wa muda mrefu uliokuwa na maneno makali, kwa mujibu wa ripoti.
Balozi
wa Urusi kwa Umoja wa Mataifa, Vassily Nebenzia alisoma nukuu ya maneno
ya Rais Vladimir Putin kwa kutekeleza mashambulizi hayo bila kuzingatia
sheria za umoja wa mataifa na bila kusubiri majibu ya shirika la
upelelezi la umoja wa mataifa linaloshughulikia silaha za kemikali la
OPCW.
Wajumbe wa OPCW wanatarajia kuzulu eneo la Douma wiki ijayo kufanya uchunguzi wa tuhuma za Syria kutumia silaha za kemikali.
Syria
imekana kutumia silaha hizo na kueleza kuwa tukio hilo limefanywa na
waasi kwa lengo la kuichonganisha serikali ya Syria na wananchi wake
pamoja na jumuiya za umoja wa mataifa. Rais Bashar Al-Assad ameseam kuwa
mashambulizi ya Marekani yanazidi kumuimarisha.


0 comments:
Chapisha Maoni