Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hana mpango wa kuwa Rais
ila anapenda kumsaidia Rais John Magufuli katika utekelezaji wa
shughuli zake.
Makonda
ameyasema hayo leo alipoulizwa na mwandishi wa Azam TV Baruan Muhuza
wakati wa mahojiano yake akielezea tathmini ya siku tano za kusikiliza
malalamiko ya wanawake waliotelekezwa na wenza wao.
Muhuza aliuliza: “Hao wote uliowasaidia wanakuona shujaa na mtu wao wa muhimu sana, unatamani kuwa rais wa nchi hii siku moja."
Makonda
amejibu,“Hapana ila natamani kumsaidia Rais Magufuli atimize azma yake
kwa wananchi hasa kwa malengo aliyonipa kwa mkoa wa Dar, hiyo ndiyo
shauku yangu."
Kuhusu
madai ya kuwachafua watu maarufu kupitia zoezi hilo amesema,
"Huchafuliwi kwa kuwa una mtoto, matendo yako uliyoyafanya ndiyo
yanayokuchafua,"
"Si
kweli kwamba eti nililenga kuwachafua wanasiasa ndiyo sababu kuna DNA.
Kama kuna mtu anafikiri ni zoezi la mtu fulani anakosea, namna pekee ya
kuepuka kuitwa kwa RC mtafute mtoto wako umlee,"
Amesema shauku yetu kubwa ni kuona kila mtoto anapata haki yake.


0 comments:
Chapisha Maoni