Na. Jeshi la Polisi.
Jeshi
la Polisi nchini limefanikiwa kukamata Silaha mbalimbali na watuhumiwa
368 katika Oparesheni Maalum inayoendelea katika Ukanda wa Kusini
unaojumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.
Akizungumza
mkoani Mtwara, Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa
Polisi Liberatus Sabas alisema kati ya watuhumiwa 368, 13 tayari
wamefikishwa Mahakamani, 152 wamekabidhiwa Idara ya Uhamiaji kwa hatua
zaidi, tisa wapo chini ya Upelelezi na 194 wapo chini ya uangalizi wa
Polisi (Police Supervisee).
Sabas
amezitaja Silaha zilizokamatwa kuwa ni pamoja na SMG mbili, Pistol
tano, Shotgun moja na risasi 145, Visu 96, Makoti ya Sare za Jeshi la
Msumbiji mawili, Raba za Jeshi la Msumbiji jozi mbili pamoja na vifaa
vya kutengenezea milipuko.
“Baadhi
ya watuhumiwa ni wale waliokimbia katika Operesheni yetu ya Mkoa wa
Kipolisi Rufiji baada ya kuwazidi nguvu na sasa nawaambia tu
wajisalimishe kwani hatuna mchezo hata wakimbilie wapi mana tumepata
taarifa kuwa wamejificha nchini Msumbiji lakini kule napo wameanzisha
operesheni kama hii“. Alisema Sabas.
Aidha
Kamanda Sabas amesema Operesheni hiyo ni endelevu na inashirikisha
vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama hivyo ametoa wito kwa raia wema
kuendelea kutoa taarifa za siri ili kuendeleza amani na usalama hapa
nchini.
Hivi
karibuni Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchini Msumbiji alikutana na IGP
Simon Sirro jijini Dar es Salaam kwa lengo kuboresha ushirikiano katika
mapambano ya uhalifu unaovuka mipaka ambayo ndio imekuwa changamoto
katika nchi mbalimbali.
0 comments:
Chapisha Maoni