Mbunge
wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo baada ya kufiwa ya mama yake mzazi usiku wa kuamkia
jana.
Zitto amesema kuwa anajua uchungu wa kupotelewa na mama huku akieleza kuwa hakuna faraja kama kumuuguza na kumsitiri mzazi.
"Pole
sana kwa Msiba huu mkubwa ndugu Mrisho Gambo. Najua uchungu wa
kupotelewa na mama. Hakuna faraja kama kumuuguza na kumsitiri mzazi.
Mola akupe subira wewe na ndugu zako. Inna lilah waina ilaih raajiun
ameandika Zitto kwenye mitandao yake ya kijamii."-Zitto Kabwe


0 comments:
Chapisha Maoni