Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda atakua mgeni rasmi wa
mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na
Yanga utakaochezwa Jumapili Aprili 29,2018 Uwanja wa Taifa Dar Es
Salaam.
Ndugu
Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu
watakaojitokeza kweye Uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo namba 178
utakaoanza saa 10 jioni.
Tayari
tiketi za mchezo huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi
30,000,VIP B na C 20,000 na Mzunguko(Jukwaa la rangi ya Chungwa,Kijani
na Bluu) 7,000.
Tiketi zinapatikana kupitia Selcom.
Katika
mchezo huo Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya
kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48
wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.
0 comments:
Chapisha Maoni