Zaidi ya familia 208 za watoto waliotelekezwa na baba zao, zimepatanishwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Paul Makonda.
Hayo
yamebainishwa jana Aprili 27 na Makonda wakati akitoa majumuisho ya
zoezi la kuwasikiliza wanawake waliotelekezwa na wenza wao wakiwa na
watoto.
Kadhalika Makonda, hakuacha kuwashukuru waandishi wa habari kwa kufanya kazi kubwa katika kuhabarisha umma kuhusu kampeni yake.
“Kwanza
niwashukuru waandishi wa habari kwa kazi nzuri mliyofanya, lakini pia
niwashukuru wote walionitukana kwa kuanzisha zoezi hili wakiwamo
wabunge,"alisema.
Alisema zoezi hilo limefanikiwa kwani familia 208 zimeanza kupata huduma kutoka kwa baba zao.
Kadhalika
amesema, kati ya watu 17,000 waliofika ofisini kwake, 90 wamefanikiwa
kupimwa uhalali wa baba kwa mtoto ( DNA) na watoto 2971 wakifanikiwa
kupata bima ya afya.
"Tumeunda
tume ya watu 15 watakaofuatilia kwa kina matatizo ya kiutawala katika
kushughulikia masuala yanayohusu jamii kwani imeonekana kuna shida
kubwa kwa watu wanaoshughulika na ustawi wa jamii," alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni