Mmiliki
wa Shule ya Sekondary ya St. Patrick ya jijini Dar es Salaam, Ndele
Mwaselela amejitolea kumsomesha mtoto wa marehemu Agnes Masogange,
Sania(11) kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne na akifaulu hadi chuo
kikuu.
Hii
ni neema nyingine kwa mtoto huyo wa pekee wa Masogange aliyemuacha,
baada ya jana kamati ya maandalizi ya mazishi kupitia mweka hazina wake,
Zamaradi Mketema kueleza kuwa wamemwekea Sh2 milioni zilizobaki katika
michango ya msiba huo kwenye akaunti yake.
Zamaradi
amesema fedha hizo zimewekwa mahususi kwa ajili ya kumsaidia kianzio
katika cha ada atakapoanza kidato cha kwanza mwakani kwa kuwa mwaka huu
anatarajiwa kumaliza darasa la saba.
Akizungumza
leo Jumatatu Aprili, 23 katika shughuli za mazishi, zilizofanyika
nyumbani kwa baba wa Masogange, Kijiji cha Utengule, Wilaya ya Mbalizi,
Mwalesela amesema mbali ya kumsomesha pia mtoto huyo atakaa hosteli kwa
gharama zake kwa muda wote wa masomo yake.
“Akifaulu
kidato cha nne pia atasomeshwa na mimi hadi kidato cha tano na sita
lakini pia akifaulu atakwenda hadi chuo kikuu,” |amesema.
Kutokana
na maamuzi hayo, alimtaka msanii Irene Uwoya ambaye mtoto wake naye
anasoma katika shule hiyo, kuhakikisha anapokwenda kumsalimia mwanaye
awe anakwenda kumsalimia na Sania.
“Hivyo
wewe msanii Uwoya una mtoto wako pale shuleni kwangu naomba ukija
kumuona hakikisha unamuona na mtoto huyo,” amesema Mwaselela
0 comments:
Chapisha Maoni