Mtangazaji
na muigizaji wa Bongo movie Lulu Semagongo maarufu kama aunty Lulu
amewaacha watu wengi midomo wazi baada ya kudai kalio lake kubwa
limemsaidia kupata wachumba watatu nchini China.
Kwenye
mahojiano na Global Publishers Aunty Lulu alifunguka na kudai kuwa
kwenye Safari yake ya kibiashara nchini China hivi karibuni alihudhuria
kwenye ukumbi mmoja ambao kulikuwa na msanii ambaye ni Mtanzania ambaye
alikuwa anapiga shoo.
Aunty
Lulu amedai baada ya muziki kuanza kupigwa alianza kucheza na kukata
mauno kiasi ya kwamba wanaume walianza kumtolea macho na usiku huo
alipata wachumba watatu ambao wapo tayari kumuoa.
"Kalio
langu limenipatia wachumba wa Kichina watatu, sasa baada ya wote
kuniambia wanataka kunioa, niliwatajia mahari yangu kuwa ni shilingi
milioni 50 na walikubali, lakini niliwapa mtihani mwingine kwamba
atakayekuwa wa kwanza kufika Bongo ndiye atakayenioa, hivyo ninasubiri
na ndoa yangu itakuwa ya mkataba”.


0 comments:
Chapisha Maoni