Kufuatia
hali hiyo, mahakama jana ilishindwa kuwasomea maelezo ya awali (PH)
rais huyo Simba ambaye anashtakiwa pamoja na makamu wake, Godfrey Nyange
maarufu kama Kaburu.
Kesi
imeahirishwa baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Takukuru, Leonard Swai
kueleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa Aveva ni mgonjwa
(very Serious) amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Swai aliomba mahakama iipangie kesi hiyo tarehe nyingine wakati wakisubiri afya ya Aveva iimarike.
Hakimu
Simba aliutaka upande wa mashtaka kuhakikisha unaandaa maelezo ya
awali, ili tarehe inayokuja waweze kusomewa PH na siku ikianza
kusikilizwa, isikilizwe mfululizo. Kesi imeahirishwa hadi Aprili 25/
2018.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi na kutakatisha fedha dola za kimarekani 300,000.


0 comments:
Chapisha Maoni