Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatarajia May 15,2018 kutoa uamuzi wa kesi ya
kufanya maandamano na mkusanyiko usio halali inayowakabili viongozi 9 wa
CHADEMA akiwemo Freeman Mbowe kama iende Mahakama Kuu ama laa.
Hatua
hiyo inatokana na mvutano wa hoja za kisheria zilizotolewa jana na
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala kisha kujibiwa leo na Wakili wa
Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard
Mashauri.
Katika
majibu yake Wakili Nchimbi ameiomba mahakama hiyo kutupilia mbali hoja
za utetezi zilizotolewa na Kibatala kwa sababu zitapelekea ucheleweshaji
wa shauri hilo pasipokuwa na sababu za msingi.
Nchimbi
amedai kuwa katika mazingira ya mwenendo wa kesi hiyo toka ilipoanza
hadi leo hakuna swali lolote la msingi lililoibuliwa na upande wa
utetezi ambalo linajikita na uvunjifu ama ukiukwaji wa haki ya kikatiba.
“Nasema
hivyo kwa sababu ukiangalia msingi wa hoja zilizowasilishwa na upande
wa utetezi jana zimejikita katika mashtaka yanayowakabili washtakiwa”
-Nchimbi
Alibainisha
kuwa ukiangalia mlolongo wa hati ya mashtaka ni hati ambayo washtakiwa
wamesomewa mashtaka zaidi ya mara moja ama mbili ikiwamo jana na
washtakiwa waliyasikia mashtaka, wakayaelewa ndiyo maana wakaenda mbele
wakayakanusha.
“Kama
kweli washtakiwa waliona mashtaka haya siyo halali, hati ya mashtaka
ilitolewa mapema hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi
zingewasilishwa kabla washtakiwa hao hawaja enterpre,” -Nchimbi.
Nchimbi
amedai kuwa washtakiwa wamefunguliwa kesi ya jinai wakati walikuwa
katika mkutano halali wa kampeni ya uchaguzi mdogo na kwamba
kuwafungulia mashtaka hayo ni uvunjifu wa haki ya kikatiba, alisisitiza
kuwa ni rai ya upande wa mashtaka kwamba yote yaliyoongelewa na upande
wa utetezi hayawezi kuitwa ni maswali ya kikatiba ambayo yangeilazimu
mahakama kupeleka kesi hiyo Mahakama Kuu.
“Hakuna
suala la kikatiba hapa na ukiendelea kufuatilia hoja za utetezi
hawajashambulia vifungu vya kisheria vilivyotumika kuwashtaki washtakiwa
hao, hivyo hoja zao hazina mashiko.” -Nchimbi
Baada
ya kutolewa kwa hoja hizo,Wakili Kibatala aliiaambia mahakama kuwa
mchakato wa kijinai ni mchakato mtakatifu ambao haukukusudiwa kuwashtaki
watu ambao wanatekeleza majukumu yao kikatiba.
Kibatala
alisisitiza kuiambia mahakama kuwa wanataka kwenda Mahakama Kuu ili
kupata tafsiri ya je ni kweli mtu akiwa anatekeleza majukumu yake ya
kikatiba ashtakiwe kijinai.
Baada
ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi May
15,2018 kwa ajili ya kutoa uamuzi kama kesi hiyo iende Mahakama Kuu ama
lah.
Mbali
na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa Mjini
Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu
Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.
Mbunge
wa Tarime mjini Esterher Matiko, Katibu wa chama hicho Dk Vicenti
Mashinji, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa Tarime vijijini, John
Heche na mbunge wa bunda, Ester Bulaya.
Washtakiwa
hao wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 12 katika kesi ya jinai namba 112
ya mwaka 2018 ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko usio halali
kinyume cha sheria na kuendelea kufanya mkusanyiko usio halali ama
maandamano yaliyosababisha kifo cha Akwilina.


0 comments:
Chapisha Maoni