Nchi ya Zimbabwe imehalalisha uzalishaji wa bagi kwa matumizi ya kiafya na kisayansi.
Zimbabwe
itakuwa nchi pili kufanya hivyo barani Afrika baada ya Lesotho, ambayo
ilitoa leseni yake ya kwanza kwa kilimo cha mmea huo mwaka uliopita.
Waziri
wa afya David Parirenyatwa amechapisha sheria zinazowaruhusu watu na
kampuni kupewa leseni ya kufanya kilimo cha bangi ambayo hufahamika
nchini humo kama mbanje, na kwamba watu wa nchi hiyo sasa wanaweza
kutuma maombi ya kulima bangi, na leseni yake itakuwa inaombwa upya kila
baada ya miaka mitano, na itawaruhusu wakulima kumiliki, kusafirisha na
kuuza bangi.
Watuma
maombi watatakiwa kueleza ni wapi watafanyia kilimo chao, kiwango
ambacho wataweza kuzalisha na kuuza na wakati wa kuzalisha bangi hiyo.
Nchini
Zimbabwe ilikuwa ni haramu kupanda, kumiliki au kutumia mmea huo nchini
Humo, na iwapo mtu atapatikana na makosa hayo anaweza kuhukumiwa
kifungo cha hadi miaka 12 jela.
0 comments:
Chapisha Maoni