Rais
Kim Jong-Un wa Korea Kaskazini amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa hilo
kuvuka mpaka wa kijeshi uliowekwa kuzitenganisha nchi hizo mbili baada
ya vita ya mataifa hayo mawili mwaka 1953. Akiwa ni mwenye tabasamu rais
Korea kusini Moon Jae-in amempokea mgeni wake katika eneo la mpakani.
Ni
miaka 65 hadi sasa kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kuwahi kuvuka mpaka
wa kijeshi uliowekwa kuzitenganisha Korea Kaskazini na Korea Kusini
tangu kumalizika kwa vita vya mataifa hayo mawili mwaka 1953.
Eneo
la mpaka huo aliouvuka Kim Jong Un wakati akielekea Korea kusini ni
lenye kilomita 250 na upana wa kilomita nne,ambapo mara baada ya kuuvuka
tu watu walipiga makofi kwa kuandikwa kwa historia.
Mkutano
huo wa tatu baada ya mkutano wa mwaka 2000 na 2007 ni matokeo ya
jitihada zilizofanyika miezi kadhaa kuimarisha mahusiano kati ya Korea
hizi mbili na kufungua milango ya mkutano kati ya Kim na Rais wa
Marekani Donald Trump.
Kim
alitangaza juma lililopita kuwa angesitisha zoezi la majaribio ya
silaha za nuklia kwa sasa.Hatua hiyo ilikaribishwa na Marekani na Korea
Kusini kama hatua nzuri,ingawa watafiti wa China wameonyesha kuwa eneo
linakofanyika jaribio la nuklia la Korea Kaskazini huenda lisitumike
tena baada ya mwamba kuporomoka baada ya jaribio la mwisho la mwezi
Septemba.
Korea Kusini na Marekani zimesema zinasitisha mazoezi ya kijeshi kwa siku moja kupisha mkutano huo.
Kim
ameongozana na maafisa tisa, akiwemo dada yake, Kim Yo-jong,aliyeongoza
ujumbe wa Korea Kaskazini kwenye michuano ya Olimpiki nchini Korea
Kusini mapema mwaka huu.Mkutano huu pia utawahusisha maafisa wa juu wa
kijeshi na wanadiplomasia.
0 comments:
Chapisha Maoni