Dj
na mtangazaji maarufu nchini Uganda Robert Ogwel maarufu kama Dj Rasta
Bob Mc amefunguka na kudai Ex wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz,
Zari alikuwa mpenzi wake kabla hajamuacha na kwenda kwa Ivan.
Dj
Rasta Bob alimwaga ubuyu huo Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni
na kituo cha Spark Tv nchini Uganda ambapo alidai yeye ndio alikuwa
mwanaume wa kwanza kuwa na Zari.
Dj
huyo amefunguka na kudai kuwa yeye ndio alimtoa Zari kwao Jinja na
kumleta jijini Kampala nchini Uganda kutokana na kuvutiwa na urembo wake
lakini pia amedai kuwa yeye ndio alimfunza mambo mengi Zari kuhusu
ustaa kwani kipindi hiko alikuwa maarufu sana.
Lakini
pia amedai muda mfupi baada ya kuwa wa mjini na kupendeza ndipo Zari
alivyomtosa na kuanza kutoka kimapenzi na mwanaume tajiri ambaye ni Ivan
na kumwambia anaweza kuishi mwenyewe mjini na kumuacha solemba.
Dj
Rasta ambaye ni mkongwe nchini Uganda katika sekta ya burudani amekiri
pamoja kuwa Zari amefanikiwa kimaisha na kutoka na wanaume matajiri
lakini watambue kuwa yeye ndio alimtoa kijijini na kumfundisha kila kitu
kuhusu kuishi mjini.


0 comments:
Chapisha Maoni