MWANAMUZIKI kiwango kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, amefunguka kwamba watu wamekuwa wakimdis kutokana na kuvaa kwake cheni yenye msalaba bila kufahamu nini anamaanisha.
Akichonga na Mikito Nusu Nusu, Diamond alifunguka kwamba
kwake huwa hachukulii cheni hiyo kama msalaba, bali ni alama ya jumlisha
ambaye kwake inamaana kubwa ambayo ni siri yake.
“Cheni ninayovaa na watu kunidisi kwamba ni msalaba
kiukweli huwa ninashangaa sana kwa maana watu huzungumza kile ambacho
hawakifahamu. Kwangu huo si msalaba, bali ni alama ya jumlisha ambayo
ninaona haina tatizo lolote, kwani alama hiyo inamaana kubwa kwangu
ambayo itabaki kuwa siri yangu!” alisema Diamond.


0 comments:
Chapisha Maoni