Mkuu
wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela amewataka vijana
kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo ili ziweze kuwanufaisha.
Ameyasema katika Tamasha la Amka Vijana la Wasanii wa filamu nchini lililofanyika katika viwanja vya Mwembe Togwa mkoani humo.
Msanii
wa muziki wa singeli, Dulla Makabila alikuwa mmoja kati ya wasanii
waliofanya vizuri hali iliyomfanya DC. Kasesela kuinuka na kuanza
kuonyesha uwezo wake wakucheza singeli jukwaani.
Katika
tamasha hilo lililofanyika hapo jana lilikuwa na lengo la kuhamasisha
vijana kujishughulisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ili wawewze
kujipatia kipato.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela amewataka vijana kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo za kimaendeleo.


0 comments:
Chapisha Maoni