Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo kimekanusha taarifa zinazoendelea
mitandaoni kuhusu uwezekano wa kurejea nchini kwa Mwanasheria Mkuu wa
Chama hicho, Tundu Lissu kutokea Ubelgiji alipokuwa akipatiwa matibabu
tangu mapema Januari mwaka huu.
Kupitia
kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Ndg. Tumaini Makene
amesema kwamba kupitia mitandaoni mapema leo kumekuwa na taarifa za
kwamba Lissu anatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania wakati wowote kuanzia
juzi, kwamba amemaliza matibabu yake kitu ambacho sicho cha kweli na
kimezua taharuki.
Katika
taarifa yake Ndg. Makene amesema kwamba Mwanasheria huyo ambaye pia ni
Mbunge wa Singida Mashariki, hajazungumza na mwandishi wa habari yeyote
juu ya kurejea kwake nyumbani kwa sababu zilizo wazi kabisa kuwa bado
hajapona na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine mwisho wiki hii au
wiki ijayo.
Hata
hivyo chama hicho kimetoa wito kwa na wanachama na Watanzania wote
wenye mapenzi mema kutokana na kuguswa na uzito wa masahibu yaliyompata
Lissu wameendelea kuguswa na kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya
matibabu na hali ya afya yake kupuuza taarifa hizo.
Tundu
Lissu yupo nchini Ubelgiji akipatiwa awamu ya tatu ya matibabu baada ya
kumaliza matibabu nchini Kenya mwezi Januari ambapo alikuwepo huko kwa
takribani miezi minne ambapo alikuwa akiuguza majeraha ya risasi.
Mbunge
huyo machachari alipigwa risasi zilizokadiriwa 37 nje ya makazi yake
huko Jijini Dodoma majira ya saa 7 mchana na watu wasiojulikana wakati
alipokuwa akitoka kwenye majukumu yake ya kibunge.
0 comments:
Chapisha Maoni