Mgunduzi
wa madini ya Tanzanite, Jumanne Ngoma ametoa ya moyoni baada ya Rais
John Magufuli kusema Serikali inautambua mchango wake na kumpa Sh 100
milioni.
Akizungumza
leo Aprili 6, wakati wa uzinduzi wa ukuta kuzungumza mgodi wa
Tanzanite, Magufuli amesema atampa barua Mzee Ngoma ya kutambua mchango
wake katika ugunduzi wa madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee.
Mzee
Ngoma alimshukuru Rais Magufuli na kusema alibaini kuwa kiongozi huyo
amechaguliwa na Mungu tangu wakati wa kampeni za urais mwaka 2015.
“Ninakushukuru
sana Rais, kwa heshima hii na kunitambua mimi kama mgunduzi wa madini,
ni heshima kubwa kwangu na niseme kuwa wewe umechaguliwa na Mungu,”
amesema na kuongeza:
“Wananchi wa Mirerani huyu ni Rais wa wanyonge, mimi nisingejulikana leo hii, hii ni furaha kubwa.”
Mtoto
wa Mzee Ngoma, Asha Ngoma naye ametoa neno katika hafla hiyo na
kumshukuru Rais kwa kuusoma na kuufanyia kazi ujumbe wake wa simu
aliomtumia Rais leo asubuhi saa 12 kasoro.
“Nikushukuru
sana kwa sababu sikutegemea kama utausoma na kuufanyia kazi ujumbe
wangu wa simu niliokutumia leo asubuhi. Naomba uendelee kuuthamini
mchango wa mzee Ngoma na kuhakikisha madini ya Tanzanite yanaendelea
kuwa na thamani,” amesema.
0 comments:
Chapisha Maoni