Wabunge
sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamepata ajali ya gari
jana usiku Machi 29, 2018 mkoani Morogoro wakati wakitokea Dodoma
kuelekea Dar es Salaam.
Baada
ya kutokea ajali hiyo saa 2 usiku katika barabara kuu ya
Morogoro-Dodoma eneo la Bwawani, wabunge hao waliumia maeneo mbalimbali
ya miili yao na kukimbizwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro.
Wabunge
hao ambao wote ni kutoka Zanzibar ni Haji Ameir Haji (Makunduchi),
Khamis Ali Vuai (Mkwajuni), Bhagwanji Maganlal Meisuria (Chwaka), Makame
Mashaka Foum (Kijini), Juma Othman Hija (Tumbatu).
Mganga
mfawidhi hospitali ya rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk Rita Lyamuya amesema
majeruhi hao walipokelewa saa 3 usiku na kupatiwa huduma za awali.
"Jana
tumepokea majeruhi sita walioumia sehemu mbalimbali na mmoja wao
alilazimika kulazwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu
(ICU) lakini hali yake inaendelea vizuri,” amesema.
“Leo asubuhi tayari tumewapa rufaa kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi zaidi.”
Dk Rita amesema Kimbe na May ndio wameumia zaidi, kupata maumivu makali.
0 comments:
Chapisha Maoni