Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum jijni Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, ameelezea
hatua inayoendelea kuchukuliwa juu ya askari polisi sita waliokuwa
wameshikiliwa kutokana na kifo cha mwanafunzi wa NIT Akwilina Akwilin,
aliyeuawa kwa risasi mapema mwaka huu
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam, Kamanda
Mambosasa amesema polisi hao bado wapo kwenye uchunguzi kubaini ni nani
anahusika, kwani mpaka sasa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa kuweza
kumbaini.
“Wale
walipokamatwa tulieleza bayana kwamba upelelezi unafanyika ili kujua ni
nani ambaye ametenda kosa lile, bado suala la upelezi linaendelea.
"Yapo maelekezo yaliyotolewa ambayo tunaendelea kufuatilia ili kuja kubaini, ikumbukwe silaha moja ambayo haijajulikana ni ipi ndio ilikwenda ikamgusa Akwilina,
lakini kama ulivyojua askari walikuwa ni wengi lakini pia kulikuwa
hakuna ushahidi kwamba yupi aliyekuwa ametenda hivyo, kwa hiyo uchunguzi
bado unaendelea”, amesema Kamnda Mambosasa.
Ikumbukwe
kwamba mnamo Februari 17, mwaka huu, mwanafuzi wa chuo cha usafirishaji
jijini Dar es salaam Akwilina Akwilini alifariki dunia baada ya kupigwa
risasi ambayo inaaminika ilitoka kwa mmoja wa askari waliokuwa
wakitawanya maandamano ya wafuasi wa chadema, huku yeye akiwa kwenye
daladala akipita njia.
0 comments:
Chapisha Maoni