Waraka
uliotolewa na Baraza la maaskofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri
chini Tanzania (KKKT) mwishoni mwa wiki iliyopita umeendelea kuibua
mjadala mkubwa nchini.
Katika
waraka wa ujumbe wa pasaka, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa
ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi.
Mambo
hayo kwa mujibu wa waraka huo ni Utekwaji wa watu ,utesaji, kupotea kwa
watu, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa
kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari MAELEZO, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali,
Dkt. Hassan Abbas, alipoulizwa msimamo wa serikali kuhusu waraka na
matamko mbalimbali ya viongozi wa dini alijibu kuwa kwa sasa serikali
haioni cha kujibu na kwamba inawatakia tu waumini kheri ya Pasaka.
Hata hivyo, Jana Rais Magufuli aliwashauri maaskofu nchini waanze kuhubiri ujenzi wa viwanda vya dawa nchini ili Tanzania isinunue dawa nje ya nchi badala ya kuishia kukosoa na kulalamika .
Alitoa kauli hiyo akiwa katika halfa fupi jijini Dar es salaam ya uzinduzi wa magari ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa ajili ya kusambaza dawa maeneo mbalimbali nchini.

0 comments:
Chapisha Maoni