Binti
Salma Abdalah ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili mkoani Mtwara
aliyekuwa akiishi Mbawala Chini, amefariki dunia kwa kujinyonga, baada
ya kukutwa na simu ambayo alipewa na mpenzi wake.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya,
amesema tukio hilo limetokea mwanzoni mwa wiki hii baada ya wazazi wa
binti huyo kuamua kumfukuza nyumbani na kumtaka kwenda kuishi kwa bibi
yake kutokana na utovu wa nidhamu, na ndipo akaamua kujitoa uhai wake.
Kamanda
Mkondya ameendelea kwa kueleza kwamba wazazi wake waligundua kuwa binti
yao alikuwa akimiliki simu ambayo hawajamnunulia, na walipomuuliza
hakuwa na jibu sahihi, ndipo baba mtu ambaye ni baba wa kufikia aliamua
kumfukuza nyumbani kutokana na kuchoshwa na tabia zake za utovu wa
nidhamu, na kuelekea sokoni kwenye biashara zake kumtafutia nauli, huku
mama yake akielekea shambani kwenye shughuli zake za kilimo,
“Ni
binti ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha pili, sasa asubuhi
baba yake wa kufikia akasikia simu ikiita kutoka chumbani kwake,
akamuambia mama yake na kumuuliza alikoipata, lakini hakuwa na jibu,
baada ya hapo wazazi wake wakatoka kuelekea shambani na kumwambia kuwa
wamechoshwa na tabia zake za utovu wa nidhamu hivyo wakirudi wasimkute
aondoke, huku nyuma akaamua kujinyonga kwa kutumia khanga”, amesema
kamanda Mkondya.
Taarifa
zaidi kutoka kwa mashuhuda wa tukio wamesema binti huyo alipojinyonga
aliacha ujumbe uliosema kwamba "Nampenda sana Daudi, siwezi kukaa naye
mbali najua hili ni kosa kwangu lakini nawaomba wazazi wangu mumpende
sana Daudi maana akiwa kwenye matatizo, mimi sitajisikia vizuri"
0 comments:
Chapisha Maoni