test

Alhamisi, 29 Machi 2018

Mbowe na Viongozi Wengine wa CHADEMA Mahakamani Tena Leo


Viongozi sita wa Chadema leo watafikishwa tena  Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa dhamana yao, huku ulinzi ukiimarishwa katika eneo hilo.

Kesi hiyo inatajwa leo Machi 29, ambapo Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard, Mashauri atatoa uamuzi kama washtakiwa hao watapata dhamana au hawatapata.

Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi kuzunguka viunga vya mahakama ya Kisutu.

Katika lango kuu la kuingia mahakamani hapo, polisi waliovalia kiraia walifanya ukaguzi kwa kila anayeingia na kutoka na kuwazuia baadhi.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni