Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimetofautiana na kauli ya
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Mwigulu Nchemba ya kutaka walimu kutumia
adhabu ya fimbo kuweka nidhamu kwa wanafunzi shuleni
Akizungumza
katika harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari Lulumba
Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Dk. Nchemba alisema walimu wanatumia
fimbo kunyoosha nidhamu za wanafunzi, ili kutengeneza hatima ya nchi.
Alisema
wakati walimu wakitekeleza majukumu yao ikiwamo kunyoosha nidhamu kwa
wanafunzi kwa kutumia fimbo, wapo baadhi ya watu wamekuwa
wakiwalalamikia na kuwataka wawaache watekeleze majukumu yao.
“Wakati
walimu wananyoosha nidhamu za wanafunzi, wapo watu wengine
huwalalamikia tu, na hawajui kwamba kinachofanyika ni kwa manufaa yetu.
"Niwaombe
kwenye kutumia mifano tumieni mifano na kwenye kutumia fimbo fanyeni
hivyo, ili kutengeneza taswira ya nchi yetu,” alisema Dk. Mwigulu.
Akizungumzia
kauli hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Hellen Kijo Bisimba,
amesema kutumia fimbo kwa mwanafunzi hakuwezi kusaidia kumjengea
nidhamu.
Pia, amesema kutumia adhabu hiyo kunaweza kuwa chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo yao kielimu.
“Ni
kweli kwamba walimu wanapaswa kuachwa watekeleze majukumu yao bila
kuingiliwa, lakini linapokuja jambo la adhabu au kujenga nidhamu kwa
wanafunzi lazima uangaliwe mfumo unaotumika,” alisema Dk. Kijo Bisimba
na kuongeza:
“Zipo
adhabu ambazo mwanafunzi anaweza kupewa akikosa, lakini si kwa kuchapwa
fimbo. Unaweza ukafikiri ukimchapa ndio unamjenga, lakini kumbe ndio
unambomoa zaidi.
"Nasema
hivyo kwa sababu unapoanza kumchapa mwanafunzi hawezi kufanya vizuri
tena darasani. Mimi namuomba waziri a-deal (ashughulike) na mambo ya
wizara yake, ya elimu ayaache.”
0 comments:
Chapisha Maoni