Chama
cha ACT-Wazalendo kimemtaka Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako aondoe kigezo cha umri walichokiweka katika
udahili wa wanafunzi kwa madai kitendo hicho kitapelekea kuwanyima elimu
watoto wa kimasikini.
Hayo
yameelezwa na viongozi wa Ngome ya vijana Taifa wa ACT jana (Machi 26,
2018) wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari katika makao
makuu ya chama chao yaliyopo Sayansi Kijitonyama jirani na Kanisa la
KKKT Jijini Dar es Salaam.
"Walichokifanya
wizara ya elimu kwa kuweka kikomo cha umri wa udahili kwenye shule za
serikali na binafsi kitapelekea kupungua wanafunzi wa elimu ya juu, kwa
kuwa kikomo hicho kitawakwamisha hasa wananchi masikini wanaoishi
vijijini na mijini katika kupata elimu. Kwenye hili tunamtaka Waziri wa
Elimu aondoe kigezo cha ukomo wa umri kwasababu kigezo hicho kina kiuka
Katiba", walisema viongozi hao. na kuongeza;
"Wametoa
kikomo hicho bila ya kuwa na tafiti yeyote ambayo wamefanya wao kama
Wizara au taasisi nyingine iliyopo nje ya serikali. Kuna athari kubwa
katika kikwazo hicho kwa maana kuna watu walichelewa kupata elimu kutoka
na maradhi, kusimamisha masomo kutokana na ada hivyo tunataka kigezo
hicho kiondolewe ili watu wa aina wasikose kupata elimu".
Kwa
upande mwingine, Viongozi hao wa Ngome ya vijana Taifa wa ACT imeunga
mkono waraka uliotolewa na Maaskofu wa Kanisa la KKKT nchini Tanzania na
kuwataka viongozi wa dini nyingine wasikae kimya wafanye kama
walivyofanya maaskofu.
“Ngome
ya vijana inawapongeza sana kwa kutekeleza wajibu wao, ushauri wa
maaskofu na maoni yao inabidi kuchukuliwa uzito wa hali ya juu,
wamezungumzia kuhusu uhuru wa kutoa maoni, mauaji ya watu, katiba mpya,
uchumi na ajira kwa vijana, ni mambo muhimu kwa watanzania wote bila
kujali tofauti zetu kuyaunga mkono,.
“Ngome inaunga mkono tamko la maaskofu kwa asilimia mia moja, serikali ichukulie kwa uzito tamko hilo na kupuuza watu wanaosema vuongozi wa dini wako kisiasa. Viongozi wengine wa dini waige mfano wao.”
“Ngome inaunga mkono tamko la maaskofu kwa asilimia mia moja, serikali ichukulie kwa uzito tamko hilo na kupuuza watu wanaosema vuongozi wa dini wako kisiasa. Viongozi wengine wa dini waige mfano wao.”
0 comments:
Chapisha Maoni