Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
ametuma salamu rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia
kifo cha Mzee Kleist Sykes kilichotokea jana tarehe 22 Novemba, 2017
Jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Rais Magufuli amesema amepokea taarifa za kifo cha Mzee Kleist Sykes
kwa majonzi na huzuni hasa akikumbuka mchango mkubwa alioutoa katika
ujenzi wa Taifa akiwa mmoja wa viongozi waliokuwa mstari wa mbele katika
kupiga vita umasikini, kuilinda misingi ya uhuru na kujenga uzalendo
kwa Watanzania.
Ameongeza
kuwa Mzee Kleist Sykes na familia yake walijitoa kwa hali na mali
kukijenga chama tangu TAA, TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi (CCM)
pamoja na kushiriki katika harakati kubwa za uhuru, kwa kuweka mbele
maslahi ya Taifa licha ya changamoto mbalimbali walizokabilina nazo.
“Mchango
wa Mzee Kleist Sykes na familia yake katika nchi yetu hautasahaulika,
uzalendo wake utakumbukwa na kudumishwa na hakika kifo chake kimetuachia
majonzi na huzuni hasa kwa kuwa kimetokea wakati ambapo busara zake
bado zinahitajika”
“Nawapo
pole wanafamilia, ndugu, jamaa, wana CCM, marafiki na wote walioguswa
na kifo hiki, naungana nao katika majonzi na sala za kumuombea Mzee
Kleist Sykes apumzike mahali pepo, Amina”
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Novemba, 2017
0 comments:
Chapisha Maoni