Kampuni
ya Udalali ya Yono imetangaza kuwa kesho, Novemba 24, 2017 itarudia
upya mnada wa nyumba mbili za kifahari za mfanyabiashara Said Lugumi
zilizoshindikana kuuzwa baada ya Dr. Louis Shika kuzinunua na kushindwa
kuzilipia.
Nyumba zilizotajwa kurudiwa kuuzwa katika mnada ni Plot. No 47, iliyopo Mbweni JKT, na nyingine iliyopo Upanga
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart,
Scholastica Kevela ameeeleza kuwa kwa sasa kampuni ya Yono imeweka
masharti magumu ili kuhakikisha kwamba hakuna atakayeibuka kuuharibu
mnada huo.
“Niwakaribishe wateja ndani na nje ya nchi kuja kujinunulia nyumba zile kwa maana ujenzi ni mgumu..” amesema.
Aidha
Bi Scholastica Kevela amewaonya wale wote wenye nia ya kuuharibu mnada
huo kutofanya hivyo kwani hawatavumiliwa na hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
“Niseme
kwamba mchezo ule tuliochezewa mara ya mwisho hautarudiwa tena. Kwa
sasa hivi tumekuja na masharti magumu kwamba washiriki wote wawe aware
na wanielewe,” amesema Bi. Kevela.
Masharti
yaliyowekwa katika minada hiyo ni kwamba mshiriki atapaswa
kujiandikisha kwenye kitabu maalum cha washiriki wa minada, baada yahapo
atajaziwa ‘commitment form’ (fomu maalumu ya kushiriki mnada).
Baada
ya hayo, vitambulisho vya mshiriki ikiwemo hati ya kusafiria
(passport), leseni ya udereva na kitambulisho cha mpiga kura
vitachukuliwa na kampuni.
Kila
mshiriki halali atapaswa kulipa kiasi cha shilingi milioni 2 kupitia
akaunti ya Yono ili kuthibitisha kuwa ana lengo la kushiriki. Kwa
atakayeshinda mnada, fedha hizo (sh. 2 milioni) zitatumika kama sehemu
ya malipo. Kwa ambao watakosa basi fedha zao zitarudishwa hapo hapo.
Kwa watakaoshiriki kuharibu mnada, hawatorudishiwa fedha hizo na watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kwa
mshindi atakayepata nyumba atatakiwa kulipa hapohapo 25% ya gharama
yote ya nyumba na 75% ya gharama inayobaki atapaswa kulipa ndani ya muda
wa siku 14.
Yono
Auction Mart wametoa onyo kubwa kwa watakaohusika kwa namna yoyote
kuharibu minada hiyo kuwa watakamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani kwa
kuwa na nia ovu ya kukwamiha ukusanyaji wa kodi ya serikali.
0 comments:
Chapisha Maoni