Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameanza kuzungushwa katika vituo vya Polisi jijini Dar es Salaam.
Zitto
baada ya kuhojiwa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe mkoani Temeke
sasa amehamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema baada ya Zitto
kuhojiwa kuhusu aliyozungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za
udiwani zilizofanyika Kijichi Jumapili Oktoba 29,2017 aliachiwa kwa
dhamana.
Shaibu
amesema Zitto aliyewakilishwa na wanasheria Venance Msebo na Steven
Mwakibolwa alidhaminiwa na watu wawili na alitakiwa kurudi kituoni hapo
Jumatatu Novemba 6,2017. Hata hivyo, amesema alikamatwa tena.
Akizungumzia
kukamatwa kwa Zitto, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,
Lazaro Mambosasa amesema kuwa wanamshikilia kwa lugha za uchochezi.
"Tunamshikilia kwa uchochezi na kutoa lugha zisizo na staha na yupo Central hapa,'' amesema Kamanda Mambosasa
0 comments:
Chapisha Maoni