Na Anitha Jonas – WHUSM
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe atakuwa
mgeni rasmi katika mkutano wa viongozi wa madhehebu ya dini wenye lengo
la kubadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali yakiwamo masuala ya
kiimani, kijamii na kiuchumi.
Taarifa
hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Lugha kutoka
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Hajjat Shani Kitogo
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya
mkutano huo.
“Sera
ya Utamaduni ya Mwaka 1999 Sura ya Nane inazungumzia Malezi na inasema
mafunzo ya dini yatakuwa sehemu ya malezi ya watoto ili kusisitiza
Maadili,Malezi Mema, Kazi, Kustahiana na Kuvumiliana,” alisema Hajjat
Kitogo.
Akiendela
kuzungumza katika mkutano huo Mkurugenzi Msaidizi huyo alisema serikali
inatambua umuhimu wa Viongozi wa Dini katika ulezi wa jamii na
maendeleo ya Taifa na ndiyo maana imeona ni vyema kukutana nao na
kujadili ni namna gani itaweza kulisimamia taifa katika kufikia malengo.
Naye
mmoja wa washiriki wa mkutano huo Bi Hadija Kisubi alitoa maoni yake na
kusema anaamini viongozi wa dini wanamchango mkubwa katika kujenga
nidhamu ya kwa taifa sababu ya neema ya mungu iliyondani ya viongozi hao
pale wanatoa maelekezo kwa umma.
Pamoja
na hayo mkutano huo umebeba Kauli Mbiu inayosema “Imani na Uzalendo
Kuelekea Uchumi wa Viwanda” na utafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere (JNICC) tarehe 25/10/2017.
0 comments:
Chapisha Maoni