Serikali
imewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na
Maafisa Mipangomiji kuweka alama za X na kuvunja majengo yote
yanayojengwa katika miji yao bila kibali na yale yanayojengwa katika
viwanja vya watu wengine walio na hati
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameyasema
hayo alipofanya ziara wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa alpoenda kutatua
mgogoro wa ardhi ambapo ameagiza eneo ya lililokuwa shamba la mifugo la
Malonje wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa lenye ukubwa wa ekari 12,750,
lirejeshwe serikalini kwa vile utaratibu wa kuligawa umekiukwa kwa
kiwango kikubwa, na masharti ya uendeshaji hayajazingatiwa kabisa.
Waziri
Lukuvi amesema tatizo la ujenzi holela lianaanza pale ambapo
Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa
Mipangomiji wanaacha majengo yanaibuka katika miji yao bila kujua ujenzi
huo una kibali au unajengwa katika kiwanja chenye hati na muhusika wa
hati hiyo ndio anayejenga.
“Hatuwezi
kuendelea na zoezi la kufanya urasimishaji wa makazi kila siku wakati
chanzo cha tatizo hilo kinajulikana, kwa hiyo naagiza Wakurugenzi,
Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka x katika
majengo yote yanayojengwa bila vibali na ujenzi unaofanywa kwenye
viwanja vya watu masikini kwa dhuruma” amesema Lukuvi.
Lukuvi
amesema atapambana na viongozi hao pale ambapo atakuta majengo
yamekithiri katika miji yao na hayana vibali vya ujenzi na baya zaidi
majengo hayo yamejengwa katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kujenga au
yamejengwa katika kiwanja cha mtu mwingine na viongozi hao wameshindwa
kufuatilia kwa kuyavunja au kuyaweka alama ya x majengo hayo, kwa kuwa
huu ni uzembe unaotokea nchi nzima.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amemhakikishia Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kuwa
atayafanyia kazi mapendekezo yake kikamilifu na kwa haraka ili kuondoa
migogoro na kero zinazoukabili mkoa wake katika masuala yote ya ardhi.
0 comments:
Chapisha Maoni