Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia...
Alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo.Nikiwa ninavua kofia,mkuu wa shule ambaye tunawindana kama paka na panya naye akawa anaingia ndani ya ukumbi huku akiwa ameongozana na mkuu wa shule.Akabaki akinitazama kwa hasira na kuanza kupiga hatua za haraka kunifwa huku mikononi mwake akiwa amekunja ngumi
Nikaanza kurudi nyuma huku nikimtazama mkuu wa shule,akazidi kuja kwa kasi ikanilazimu kusimama nikimtazama kwa umakini.Wanafunzi wote wakawa na hamu ya kuangalia ni nini ambacho atakifanya mkuu wa shule.Hatua chache kabla hajanifikia nikaifunua tisheti yangu sehemu ya kiunoni na kumuonyesha bastola niliyo ichomeka kiunoni.Kidogo akapunguza kasi hadi ananifikia munkari wote ulimuishia.
“toka katika shule yangu”
Alizungumza huku meno yake ameyang’ata kwa hasira.Nikamtizama na macho makali na ukumbi mzima wa shule upo kimya hata kijiko kikianguka mlio wake utasikika vizuri.
“sitoki”
Wanafunzi wote wakashangilia,mkuu wa shule akawatizama wanafunzi na wakakaa kimya
“walinzi mupo wapi?”
Mkuu wa shule alizungumza kwa sauti kubwa,hapakuwa na mlinzi hata mmoja aliye nifwata kila mlinzi aliye niona kuwa ni mimi aliishia mlangoni na kusimama.Mmiliki wa shule akatufwata sehemu tulipo simama na mkuu wa shule
“jamani,kuweni wapole.Mkuu unaniambisha bwana”
Mkuu wa shule akajifanya kama hamsikii muajiri wake,kitu kinacho niumiza kichwa ni kwanini mkuu wa shule hadi leo yupo wakati amafanya mambo ya ajabu hadi muda huu hajachukuliwa hatua zozote.Akanisogea katibu yangu,nikastukia kibao kikali kikitua kwenye shavu langu.Nikataka kulipiza nikaisikia sauti ya john ikiniita jina langu na nilipo mtizama nikamkuta john akitingisha kichwa akiniashiria nisifanye chochote
Mkuu wa shule akanitandika kibao cha pili,ila john akawa na kazi moja ya kuniomba hadi machozi yakawa yanamwagika,nisilipize chochote kwa mkuu wa shule.Machozi ya hasira yakaanza kunimwagika,huku kifua changu kikianza kutanuka kwa hasira kali,akataka kunitandika kofi la tatu nikamdaka mkono wake.
“nitakuua”
Nilizungumza kwa sauti ya ukakamavu,huku macho yangu yakimtazama mkuu wa shule.Akajaribu kuuchomoa mkono wake kutoka kwenye mkono wangu ila akashindwa.John kwa haraka akaja na kuingia katikati yetu na kuniachanisha mkono wangu na mkuu wa shule na kunishika mkono na kuanza kunitoa nje
“eddy achana naye huyo mzee”
Machozi yakazidi kunimwagika,pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote
“john niachie,tafadhali”
“eddy siwezi kukuachia,nakujua.Tuliza kwanza hasira”
“john,yule mzee ananitafuta nini mimi?”
“mpotezee bwana,hajui atendalo”
“john,mama yangu hata siku moja hajawahi kunizalilisha mbele ya watu kwa kunipiga.Sembuse yeye kikaragosi”
“ndio,naelewa hilo eddy ila punguza jazba”
Tukaingia kwenye moja ya darasa lililopo chini ya ukumbi kwani ukumbi upo gorofani.John akanikalisha kwenye moja ya kiti na yeye akakaa mbele yangu juu ya meza.Moyo na mwili wangu vyote vikawa vinajisikia vibaya sana kwa kitendo cha kuzalilishwa.Kwani katika maisha yangu tangu nikiwa mtoto sikupenda mtu kunizalilisha wala kunionea.
Hata awe ni mkubwa vipi nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kupambana naye hata akinipiga basi ipo siku nitamvizia hata kwa mawe nimpige,ndio maana hadi hapa nimekua bondia mzuri tuu.Nikaichomoa bastola yangu kwa haraka john akanibeta na kunipokonya
“eddy,unataka kufanya nini?”
“lete hiyo bastola”
“ahaa eddy sikupi”
John alikimbia nyuma ya darasa,huku bastola akiwa ameishika mkononi.Nikamtazama kwa macho makali sana yasiyo pepeseka hata kidogo.Kwa haraka nikatoka mlangoni na kumfungia john kwa nje.Nikakimbia na kuanza kupandisha ngazi za kuelekea kwenye ukumbi.Kitendo cha mguu wangu wa kwanza kukanyaga sakafu ya ukumbini nikatazama wapi alipo mkuu wa shule.
Nikamuona akiwa amekaa kwenye meza ya wageni waalikwa akiwa katikati ya waalimu wengine na mmiliki wa shule.Kwa kasi ya ajabu nikakimbia hadi alipo kaa na kujirusha na sote wawili tukaanguka na kiti,mbaya zaidi yeye akangukia mgongo na kunipa mimi nafasi nzuri ya kumkalia kwenye kifua chake na kuanza kumshambulia kwa ngumi zisizi na idadi kwenye uso wake
Kelele za wanafunzi kushangilia zikazidi kuongezaka,waalimu walio karibu yetu wakaanza kunivuta,kuniachanisha na mkuu wa shule.Wakanisimamisha na kunipeleka pembeni.Mkuu wa shule akasimaa huku akitaka kunifwata ila waalimu wezake wakanizuia.Ukumbi mzima wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita wakawa na kazi ya kunishangilia huku wakilitaja jina langu na kupiga makofi.
“eddy......Eddy........Eddy........Eddy”
Mkuu wa shule akawazidi nguvu,waalimu walio mshika na kuja kutuvaa na waalimu ambao wamenishika mimi.Sote tukaanguka chini,kabla mkuu wa shule hajafanya chochote nikamuwahi kumdaka shingo na kumpiga kabali.Akaanza kunishindilia ngumi za mbavu,nikamuachia shingo yake na kumsukuma pembeni na kunyanyuka juu kidogo.Akanyanyuka kwa kasi na kunifwata,kabla hajanifikia nikaruka juu kwa kutumia mguu wangu wa kulia,nikautulisha kwenye kifua chake na kumuangusha chini.Waalimu wakaendelea kutushika,kelele za wanafunzi wezangu zikazidi kuongezeka.Hata ambao wawanijui vuzuri,nao pia wakawa katika mkombo wa kushangilia
“nitakuua wewe kijana”
Mkuu wa shule alizungumza huku akiwa ameshikwa na wezake kwa nguvu.Nikabaki nikitabasamu kwa dharau zaidi nikamnyooshea kidole cha kati kama tusi.Ndio nikawa nimemfungulia hasira zake zote.Akajibabadua mikononi mwa waalimu wengine na kunifwata.Nikasikia mwalimu mmoja aliye nishika akiwaambia wezeke
“hembu muachieni tuone atakacho kifanya,mzee mgomvi kama nini”