Mhe. Mbilinyi amesema hayo baada ya kumtembelea Tundu Lissu juzi jijini Nairobi nchini Kenya na kueleza kuwa afya yake inaimarika kila siku tangia ashambuliwe kwa risasi.
“Nimemtembelea ‘Big hommie’, Nairobi hospital. Ameniambia nikawaambie wana Mbeya kuwa alisikia mwitikio wao wa kishindo nilipomtaja kwenye jukwaa la muziki na kuwa mwili wake ‘uliovunjwa vunjwa’ kwa risasi unazidi kuimarika na atasimama tena. Ameniagiza niwaambie wana Mbeya na Watanzania wote wajiandae, wajiandae, wajiandae” ameandika Mhe. Joseph Mbilinyi kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Juzi Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini walimtembelea Tundu Lissu jijini Nairobi, Kenya anapopatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma Septemba 7, mwaka huu
0 comments:
Chapisha Maoni