Aliyekuwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema amezungumzia kauli
yake ya mwaka 2014 ya kumuita ‘tumbili’ aliyekuwa mbunge wa Kigoma
Kusini, David Kafulila wakati wa mjadala wa Escrow bungeni, ambapo
amesema ulikuwa msemo tu.
Jaji
Werema ametoa ufafanuzi wa kauli yake ikiwa ni siku moja baada ya Rais
John Magufuli kumsifu Kafulila kwa kuibua sakata la akaunti ya Tegeta
Escrow na kumueleza kuwa yeye ni mtu safi na kwamba waliomuita tumbili
ndio watakaokuwa tumbili.
“Unajua
wengi walishindwa kuelewa nilisema nini, mimi nilichokizungumza ni
kwamba tumbili haamui mambo ya msituni. Na huo ni msemo wa kawaida tu,”
Jaji Werema anakaririwa na Mwananchi.
Hata
hivyo, alikataa kuzungumzia kwa undani kuhusu kauli hiyo na sakata la
Escrow akieleza kuwa watuhumiwa wa sakata hilo tayari wameshafikishwa
mahakamani hivyo sio jambo jema kujadili suala hilo.
Mwaka
2014, kulitokea mvutano bungeni baada ya kafulila kuibua sakaka la
Escrow ambapo Jaji Werema akiwa mwanasheria mkuu wa serikali alipinga
vikali maelezo ya Kafulila akidai kuwa hajui anachokisema. Werema
alimuita Kafulila ‘tumbili’, lakini mbunge huyo wa Kigoma Kusini alijibu
kwa kumuita ‘mwizi’ huku akitaka uchunguzi ufanyike ili ifahamike ‘nani
ni tumbili na nani ni mwizi’.
Kwa
mujibu wa ripoti ya kamati maalum ya bunge, jumla ya shilingi bilioni
306 zilitolewa kinyamela katika akaunti maalum ya ‘Tegeta Escrow’
iliyokuwa imefunguliwa kwa pamoja na Tanesco na kampuni ya kufua umeme
ya IPTL, ikisubiri usuluhishi wa Mahakama na ukokotoaji.
Hivi
karibuni mmiliki wa kampuni ya VIP Engineering, James Rugemarila ambaye
pia ni mmiliki mwenza wa kampuni ya IPTL pamoja na Mwenyekiti wa PAP,
Habinder Seth Sigh wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya
uhujumu uchumi. Wawili hao wako rumande kutokana na mashtaka yao
kutokuwa na dhamana.
0 comments:
Chapisha Maoni