WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kuhakikisha kwamba programu
zote zinazotolewa na taasisi za elimu ya juu zinawawezesha wahitimu
kujiajiri na kuwa na sifa za ushindani katika soko la ajira kimataifa.
Amesema
wakati umefika sasa kwa wasomi katika vyuo vyetu vikuu tujiridhisha
kuwa mitaala inayotolewa kama inawaandaa wahitimu kupata taaluma na
stadi za kuweza kujiajiri na kupambana na changamoto za kimaisha.
Amesema
taasisi za elimu ya juu nchini ziangalie mitaala yake na kuimarisha
mfumo wa ithibati na udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo ili kwenda
sambamba na dunia ya kazi inayoendana na agenda ya maendeleo ya Taifa.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo jana (Jumatano, Julai 26, 2017) wakati wa
ufunguzi wa maonesho ya 12 ya Elimu ya Juu, jijini Dar es Salaam ambapo
amevutaka vyuo hivyo badala ya kuendelea kulumbana kwenye makongamano na
vyombo vya habari, vifanye maboresho yanayotakiwa ili viweze kuendelea
na ufundishaji.
Aidha
alisema kuwa, lengo la serikali ni kuhakikisha elimu inayotolewa
inakuwa bora na kwamba maboresho yanayotakiwa kufanyika yanawezekana.
Waziri
Mkuu alisema maonesho hayo ni jukwaa la kipekee ambalo litaibua mjadala
sahihi kuhusu uhalali wa kozi zinazotolewa na vyuo husika vya elimu ya
juu. “Hivyo mnayo nafasi ya kuonesha kwa vitendo uwezo wenu katika
utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia zinazotumika
katika maendeleo ya viwanda.”
Alisema
ni vema mfumo wa ithibati na udhibiti wa ubora wa elimu na mafunzo
ukaimarishwa ili kuhakikisha asilimia 60 ya wanafunzi wanahitimu shahada
kwenye sekta ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi.
Alisema
taasisi za elimu ya juu ziweke mikakati ya kuinua na kuboresha taaluma
wanayoitoa ili ilete tija kwa maendeleo ya Taifa na Dunia. Pia kuanzisha
program za mafunzo zenye kukidhi mahitaji na kuleta maendeleo ya
kijamii na kiuchumi kwa kuzingatia mahitaji ya kitaifa, kikanda na
kimataifa.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amezitaka taasisi hizo kuendelea kuimarisha mfumo wa
udahili na kujipanga kutumia fursa za elimu na mafunzo ndani na nje ya
nchi kwa makundi yote ya jamii kwa usawa katika ngazi zote hususan
ufundi, hisabati, sayansi na teknolojia.
Pia
Waziri Mkuu alisema ni wakati muafaka kwa taasisi za elimu ya juu
nchini kuandaa mikakati ya kuongeza udahili kwa kuzingatia mahitaji ya
rasilimali watu na ujuzi unaohitajika katika sketa zinazokua haraka
mfano mafuta, gesi na madini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, JULAI 26, 2017
0 comments:
Chapisha Maoni